TANZANIA: Walichokubaliana Barnaba Na Vanessa Mdee, Kila Mwaka Watakifanya

Msaani wa Bongo Flava, Barnaba amefunguka sababu ya kufanya ngoma nyingine na Vanessa Mdee.

Muimbaji huyo amesema kuwepo kwa muendelezo wa ngoma kati yake na Vanessa ni moja ya makubaliano yao kimuziki.

“Chausiku ni mwendelezo wa 'Siri' lakini ni aina yake, kwenye ladha yake na kwenye muonekano wake tofauti. Lakini mimi na Vanessa tuna makubaliano ya kufanya ngoma moja kila mwaka,” Barnaba ameiambia EATV.

Hadi sasa Barnaba na Vanessa Mdee wametoa ngoma mbili, wimbo wa kwanza ‘Siri’ ulitoka mwaka na wa pili ambao ndio mpya kwa sasa unaitwa Chausiku.

Source: bongo5.com

Leave your comment