TANZANIA: Kwa Wanawake ni Kujiamini Ili Kufanikiwa – Rosa Ree Katika Siku ya Wanawake Duniani

Katika kuhadhimisha siku ya wanawake duniani msanii wa muziki Bongo, Rosa Ree ameeleza vitu ambavyo vitawawezesha wanawake wenye vipaji kuweza kufanikiwa.

Rapper huyo anayetamba na ngoma ‘Marathon’ ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa wanawake wanapaswa kujiamini, kuamini wanachofanya na kuwa na bidii.

“Kwa wanawake wote wenye vipaji ni kujiamini, unatakiwa ujiamini ili uweze kukamilisha ndoto,” amesema.

“Pili ni kuwa na imani kwenye kitu ambacho unakifanya, tatu ni kutia bidii, huwezi kuwa na ndoto halafu hutii bidii ili kuweza kukamilisha malengo yako,” amesisitiza.

Hapo kesho, March 9, 2018 Rosa Ree anatarajia kuachia video ya ngoma yake inayokwenda kwa jina la Marathon ambayo amemshirikisha Bill Nass.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news