TANZANIA: Muziki Ni Zaidi Ya Lugha – Young Dee

Msanii wa Bongo Flava, Young Dee amedai kuwa muziki ni zaidi ya lugha hivyo si kweli wao kuimba tu Kiswahili kunakwamisha muziki huo kufika mbali kimataifa.

Rapper huyo na hitmaker Wa ‘Bongo Bahati Mbaya’, amesema kuna wasanii wa nje wanafanya vizuri hapa Bongo lakini hatuelewi wanachoimba.

“Muziki ni kitu universal ndio maana kuna watu wanapenda nyimbo za kina Beyonce, Jay Z, Shakira, bila hata kuelewa nini wanaimba. Kama Cabo Snoop  kulikuwa hakuna hata mtu anamuelewa lakini walikuwa wanapenda kile anachofanya,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“Kwa hiyo muziki ni zaidi ya hivyo, muziki ni jinsi gani unaweza ukaimba kitu kikawa universal na kumfanya mtuo yeyote ambaye hajui lugha yoyote akaelewa, hapo utakuwa amefanikiwa,” ameisisitiza.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news