TANZANIA: Dogo Janja Kufanya Biashara na Watoto

Msanii wa Bongo Fleva, Dogo Janja amefunguka kwa  kusema kuwa yeye hana mpango wa kufanya biashara ya nguo kama wasanii wengine bali anafikiria kuwa na bidhaa za michezo za watoto.

Dogo Janja ameimbia show ya XXL ya Clouds Fm kuwa amejipanga kuja na brand ambayo itatoa vitu vya watoto kama game.

“Yaani mimi nitakuwa na deal na madogo, madogo janja Mungu akijalia niweze kusafiri nikaenda kuifanyia mitikasi hiyo nikirudi hapa narudi na bidhaa.  Unajua ukifanya biashara na mtu mzima haitamuhusisha mtoto, lakini ukifanya biashara na mtoto itamuhusisha mtu mzima,” amesema Dogo Janja.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news