TANZANIA: ‘Rama Dee’ Ataja Vitu Vinavyompa Furaha na Huzuni Maishani Mwake

Msanii wa muziki wa R’n’B nchini Tanzania, Rama Dee ametaja vitu viwili ambavyo katika maisha yake huwa vinampa huzuni na furaha kila anapovikumbuka.

 

Rama Dee amesema katika maisha yake kifo cha Mama Yake mzazi huwa kinamuumiza sana akilini ingawaje kilitokea miaka mingi iliyopita lakini huwa anaumia sana kwani alikuwa ni nguzo muhimu maishani mwake.

Mimi kitu kinachonipa huzuni katika maisha yangu ni kifo cha Mama yangu mzazi nilimpenda sana kwani alikuwa ni kama rafiki yangu“Alisema Rama Dee kwenye kipindi cha Kikangooni cha EATV.

Kuhusu ni kitu gani kinachompa furaha maishani mwake amesema ni kuwa na watoto wenye afya  na familia yake kiujumla kwani huwa akiwa nayo daima hujiona mwenye bahati.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news