TANZANIA: Hanscana Asema Ujio Mpya wa Darassa

Muongozaji wa video za bongo Hanscana ambaye ni mtu wa karibu wa Rapa Darassa amefunguka na kusema kuwa wiki ijayo rapa huyo ataachia video ya ngoma yake mpya ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki zake walio wengi.

Hanscana alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Frida Night Live (FNL) na kusema si kawaida kwa Darassa kuweka wazi mambo yake lakini kwa bahati mbaya yeye ameweka wazi ujio wa video mpya wa msanii huyo ambayo inatarajiwa kuachiwa wiki ijayo. 

"Haikutakiwa kabisa mimi kusema lakini ndiyo hivyo bahati mbaya nimesema kwa hiyo Darassa anaachia video yake mpya na ngoma mpya wiki ijayo" alisema Hanscana

Darassa mpaka sasa bado anaendelea kufanya vyema na wimbo wake 'Muziki' ambao umepata mafanikio makubwa sana katika historia ya muzuki wa Darassa na kumletea mafanikio makubwa kuliko hata nyimbo zake nyingine nyingi alizowahi kuzitoa. 

Source: eatv.tv

Leave your comment

Other news