TANZANIA: Huu Ndio Ujumbe wa Diamond Kwa Ray C

Kurudi tena kwa Ray C katika muziki kumewafurahisha mashabiki wengi ambao walitamani kusikia sauti ya kumtoa nyoka pangoni kutoka kwa mrembo huyo.

Diamond ni mmoja wa mashabiki hao ambao – hitmaker huyo wa Marry You, kupitia mtandao wa Instagram ameamua kuweka wazi jinsi alivyofurahi Kurudi tena kwa msanii huyo huku akizidi kumpatia moyo wa kutokata tamaa.

Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali…. Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya…. Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku @rayctanzania

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news