TANZANIA: Albamu ya Barnaba ni Moto, Imewakutanisha Maproducer Hadi wa SA!

Barnaba amedai albamu yake mpya imewakutanisha watayarishaji wa muziki kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Hitmaker huyo wa Lover Boy, ameiambia Bongo5, ukiachana na Tuddy Thomas, Dee Classic na Chizan Brain kushiriki kuiandaa albamu hiyo pia imewakutanisha maproducer wengine kutoka Afrika Kusini, Kenya na sehemu nyingene.

“Albamu yangu imewashirikisha maproducer wengi wengine wanatoka South Africa, Kenya na sehemu nyinge mbalimbali, lakini pia kuna wale wengine wanaitwa mateacher wao wanakuja kukaa studio tu nao wana mchango wao pia,” amesema Barnaba.

“Albamu itatoka mwezi ujao, tunataka kabla ya mwezi wa tano iwe tayari imeshatoka,” ameongeza.

Source: bongo5.com

Leave your comment