TANZANIA: Gharama Nilizotumia Kushoot Video ya 'Phone' Haina Tofauti na Kama Ningeenda Kufanyia SA - Ben Pol

Ukiongelea video kali za Bongo Fleva tulizozishuhudia tangu mwaka huu uanze, lazima utaitaja video ya Phone ya mfalme wa Rnb,Ben Pol. Ben Pol amefunguka kupitia Supermega ya Kings Fm kuwa video hiyo aliamua kuifanya kitofauti na video zake za nyuma.

“Vitu vyote vilifanywa na watu,mimi niliamua kuwa professional kuwapa watu kazi ya ku-organise location,model na vitu vyote,”amesema Ben Pol.

Kuhusu gharama zilizotumika kukamilisha kichupa hicho,Ben Pol amedai kuwa japo hajapiga hesabu kamili mpaka sasa,lakini ni video iliyogharimu pesa nyingi sawa na gharama za kufanya video nje ya nchi.
“Ukitoa gharama za ndege na hoteli,gharama zingine zimeenda sawa na video za nje,”amesema Ben Pol.

By Prince Ramalove
Kings Fm.

 

Credits: bongo5.com

Leave your comment

Other news