TANZANIA: Madawa ya kulevya yamuathiri mshiriki wa Big Brother Nando

 

 

 

 

Staa aliyewahi kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa – The Chase, Nando ameendelea kudhoofika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya

Nando aliyewahi kudai kuachana na matumizi ya dawa za kulevya, alikuwa kipenzi cha wasichana wakati anashiriki kwenye shindano hilo na alitazamiwa kushinda kabla ya kutimuliwa kutokana na kujihusisha kwenye ugomvi kwa kumtishia kumchoma kisu mshiriki wa Ghana.

Mwishoni mwa wiki, picha inayoonesha muonekano wake wa sasa imesambaa mtandaoni na kuwashtua watu wengi.

Mwaka uliopita staa mwingine aliyeiwakilisha Tanzania katika shindano hilo, Feza Kessy, alisema kuwa anaamini Nando amepatwa na tatizo au anaugua kwakuwa tabia anazozionyesha zinampa mashaka.

Akiongea kwenye kipindi cha Kubamba kupitia Times FM, Feza alisema anaona akili ya Nando kama imevurugika kwa sasa. Alisema amekuwa tofauti na Nando, yule kijana mwenye nidhamu na mpole aliyekuwa akimfahamu.

“Naamini Nando ana tatizo asaidiwe,” alisema Feza. “Sijui kwanini lakini naamini Nando ana something hayupo sawa, sio yule Nando ninayemfahamu, naomba atafutwe asaidiwe,” alisisitiza.

Feza ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa Choice FM, alidai kuwa aliwahi kukutana na Nando na akampa noti ya shilingi elfu 10. Anasema badala yake yake staa huyo aliitupa chini kwa madai kuwa haiwezi kumsaidia kitu.

Kabla ya hapo Nando aliwahi kudai kuwa atatoa kitabu chake kiitwacho ‘Mhuni huyo Mwenye Akili.

“Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu mwanangu…unajua ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema. Na peer pressure na watu niliokuwa nao wakati ule, na life niliyoishi mimi…ni yale maisha ya kujiachia,” Nando alikiambia kipindi cha Hatua Tatu cha Times FM kuhusu kilichomfanya ajiingize kwenye matumizi ya dawa hizo

 

source: bongo5

Leave your comment

Other news