TANZANIA: Songa anakwenda alipo Darasa – Nay Wa Mitego

 

 

Rapa Nay Wa Mitego ambaye kwasasa ameachia wimbo wake 'Sijiwezi', amefunguka na kumtabiria makubwa Rapper Songa baada ya kusikia kazi yake mpya 'iitwayo 'Ni mwendo tu'

 

Nay Wa Mitego alisema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kuwataka wasanii wa Hip hop kubadilika na kuweka misingi pembeni ili waweze kufanya muziki wa biashara ambao unaweza kuwafanya wabadilishe maisha yao 

 

"Nimesikiliza na kuiona ngoma mpya ya Songa kiukweli nimeiipenda naona Songa anakwenda alipo Darassa sasa safi sana, tufanye muziki wa pesa kama hivi mambo ya misingi sijui tuiweke pembeni" alisema Nay wa Mitego. Unaweza kujipatia kibao hicho kupitia app yako ya Mdundo.

Leave your comment