NEW VIDEO (TANZANIA)- ‘Don’t Bother’ ya Joh Makini Ft AKA kutambulishwa MTV Base Nov 10

 

Kwa miezi kadhaa iliyopita Joh Makini wa kundi la weusi alikuwa Afrika kusini alipokuwa akishoot video na A.K.A wa nchini humo ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Don’t Bother’. Wiki iliyopita Nikki wa Pili wa kundi hilo pia alitambulisha wimbo wake wa 'Baba Swalehe' na sasa ni zamu ya Joh Makini kuwaonyesha mashabiki wake wa Tanzania na Afrika kwa ujumla kazi yake mpya aliyoifanya nje ya Tanzania.

Video ya wimbo huo itatambulishwa kwa mara ya kwanza leo Novemba 10 saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na kituo cha Televisheni cha kimataifa cha MTV Base.

‘Don’t Bother’ imetayarishwa na Nahreel wa The Industry, na video imeongozwa na Justin Campos wa Afrika Kusini.

Kundi hilo la weusi waliahidi baada ya uchaguzi kuachia nyimbo zao kwa kupishana siku chache chache, baada ya Nikki wa Pili amefata Joh Makini na sasa bado G Nako ambaye pia ana video mpya aliyoifanya Afrika Kusini na kuongozwa na Campos.

Leave your comment