[Verse 1]
Tabu sio kupata penzi
Tabu kupata bora mpenzi
Mwenye kujua matunzo
Tabu sio kupata penzi
View moreTabu kupata bora mpenzi
Mwenye kujua matunzo
Mwenzenu nyuma nilidanganyika kwa kijana
Akanijaza kwa sana
Si ndo nikaona hili ndo bwana
Nilizama pasipozamika
Ona nikadidimizika
Ila sikujali, nilijipa moyo nikimuomba Mungu
Mbele ya safari nilijipa moyo ntampata mzuri tu
Mwenzenu nyuma…
Oh mwenzenu nyuma…
Wacha niseme maana yamenifika shingoni
Nakosa unene amani sina moyoni
[Chorus]
Sijutii kukufahamu nimejifunza mengi eh
Wacha niseme maana yamenifika shingoni
Nakosa unene amani sina moyoni
Sijutii kukufahamu nimejifunza mengi eh
Nimejifunza mengi eh
[Verse 2]
Mto wenye mamba wengi
Ni huo huo wenye samaki wengi
Inabidi niingie nivue eh
Mwenzenu nyuma nilidanganyika na kina
Nikajazwa sana si ndo nikaona nimepata
Nilizama pasipozamika, ona nikadidimizika
Ila sikujali nilijipa moyo nikimuomba Mungu
Mbele ya safari nilijipa moyo nitampata mzuri tu
Nilichimba kisima, kata ikanidumbukiza mwenyewe
Nilichimba kina, mwisho nikadumbukiaga mwenyewe
[Chorus]
Sijutii kukufahamu nimejifunza mengi eh
Wacha niseme maana yamenifika shingoni
Nakosa unene amani sina moyoni
Sijutii kukufahamu nimejifunza mengi eh
[Outro]
Sijutii kukufahamu (moyoni)
Sijutii kukufahamu
Wacha niseme maana yamenifika shingoni
Nakosa unene amani sina moyoni
Sijutii…
Leave your comment