Lyrics
Naanza kwa jina, la mola muweza
Kumsifu tumwa, kipenzi cha yeye
Naanza kwa jina, la mola muweza
Kumsifu tumwa, kipenzi cha yeye
View more
Sifa za rasuli, hazina kifani
Zimemiminika, hizo sifa zake
Sifa za mtume, hazina kifani
Kamsifu RABBI, jala rahmani..ALLAH
Sifa za rasuli, hazina kifani
Zimemiminika, hizo sifa zake
Sifa za mtume, hazina kifani
Zimemiminika hizo sifa zake
Kamsifu RABBI, jala rahmani
Hakuna mwengine, ila ni Muhammad
Sifa za rasuli hazina kifani
Hapa twazitaja sifa kwa uchache
Sifa za mtume hazina kifani
Hapa twazitaja sifa kwa uchache
Mzuri wa sura, umbo na tabia
Amekamilika, mtume Muhammad
Sifa za rasuli hazina kifani
Zimemiminika hizo sifa zake
Sifa za mtume hazina kifani
Kamsifu RABBI jala rahmani (ALLAH)
Jua nimmpole, pia nimkweli
Ni muaminifu, kipenzi wa ALLAH
jua nimmpole pia nimkweli
Ni muaminifu kipenzi wa ALLAH
Si mwenye hasira, ni mwenye subira
Katakaswa moyo, mtume Muhammad
Sifa za rasuli hazina kifani
Zimemiminika hizo sifa zake
Sifa za mtume hazina kifani
Kamsifu RABBI jala rahmani ALLAH
Yeye ni mmbora, wa mitume yote
Tuliyoshushiwa na mola jalia
Yeye ni mmbora wa mitume yote
Tuliyoshushiwa na mola jalia
Yeye ni wa kwanza, na ndie wa mwisho
Hakuna mwengine ila ni Muhammad
Sifa za rasuli hazina kifani
Zimemiminika hizo sifa zake
Sifa za mtume hazina kifani
Kamsifu RABBI jala rahmani
Jua tumeumbwa kwa nuru ya tumwa
Bila ya Muhammad tusingekuwepo
Jua tumeumbwa kwa nuru ya tumwa
Bila ya Muhammad tusingekuwepo
Tumswalieni kiongozi wetu
Muombezi wetu siku ya kiyama
Sifa za rasuli hazina kifani
Zimemiminika hizo sifa zake
Sifa za mtume hazina kifani
Kamsifu RABBI jala rahmani ALLAH
Sifa za rasuli hazina kifani
Zimemiminika hizo sifa zake
Sifa za mtume hazina kifani
Zimemiminika hizo sifa zake