TANZANIA: Nilikuwa nafanya kazi kwa Donald Trump - Wakazi

 

 

 

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Wakazi amedai wakati yuko masomoni nchini Marekani alishawahi kufanya kazi kwenye Hoteli ya mgombea Urais wa sasa wa nchi hiyo kupitia chama cha Republican, Donald Trump.

Rapper huyo amedai kazi ya hoteli ni kazi ambayo ilimpa nafasi ya kukutana na mastaa wengi zaidi wakiwemo Kanye West, Floyd Maywether, Diddy na Wengine Kibao.

“Nilikuwa tu Door man (Mfungua milango) shughuli zangu ni Front Desk, kwa hiyo nikapata kazi Trump Tower ya Donald Trump, yeye mwenyewe aliwahi kuja siku ile tu inafunguliwa ila watoto wake nimeshakutana nao sana” Wakazi alikiambia kipindi cha Campus Vibes cha Times FM.

Wakazi aliendelea kusimulia kuwa tabia kubwa ya Bilionea Trump, ni kusoma Magazeti kila siku alfajiri saa 11 na dakika 45, hivyo alikuwa akitumwa kumpelekea Magazeti Chumbani kwake kila siku asubuhi lakini kwa masharti ya kutokushikana mikono.

“Nilikuwa nampelekea Magazeti kila siku saa 11 ukifika hamuongei wala kushikana mikono, anafungua milango alafu wewe unayaweka chini, ilikuwa ni tabia yake huwa hapendi Kushake ‘hands’.”

Katika hatua nyingine rapa huyo ameongeza, kuna kipindi aliamua kuacha kazi kwa tajiri huyo ili ajihusishe zaidi na muziki huku mcheza kikapu mtanzania Hashim Thabeet akimsaidia baadhi ya mahitaji.

Source: Times FM

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment