TANZANIA: "I can't leave hip hop alone" - Mr Sugu

 

Mbunge wa mbeya mjini kupitia chama cha democrasia na maendeleo Chadema Joseph Mbilinyi kama anavyo fahamika Mr II Sugu anataka kurudi katika ‘game’ ya muziki wa bongo fleva. Mbunge huyo ambaye sasa ameingia muhula mwingine bungeni mara baada ya kupata kura za kutosha uchguzi mkuu wa octaba 2015

Kupitia ukurasa wake wa instagram ameweka post ambayo inamuonesha anarudi katika ‘game’ la muziki baada ya kukaa nje kwa miaka mitano bila ya kutoa ngoma yoyote.

 

 

Amesema kuwa “I cant leave Hip Hop alone” kisha juu katika ‘cover’ anaonekana SUGU FT LIZZY ngoma hiyo amefanyia MJ record producer.

Mr Sugu katika mahojiano yake kwenye Amplifaya ya Clouds Fm amesema kuwa, “Mimi bado mwanamuziki hata juzi nilikuwa studio narekodi ngoma mpya ambayo itasikika hivi karibuni, zamani tulikuwa tunajivunia mistarii lakini sasa hivi ni mambo ya Branding tu, kutoa video kali basi, nimeona ngoma mpya ya Fid Q amebadilika na amejaribu kuendana na muziki wa sasa unavyotaka” .

 

Leave your comment