TANZANIA: "Tusimdharau Chidi Benz" – Fid Q

 

Rapa mahiri nchini Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q amefungukia suala la rapa anayefananishwa nae kimichano maarufu kama Stamina kukanusha kujiita Chid Beenz.

 

Stamina

 

Akizungumzia suala hilo katika mahojiano yake na kipindi cha Planet Bongo ya East Afrika Radio rapa huyo amesema hashangai watu kumfananisha na Stamina kimashairi na kuongeza kuwa kila mtu anatambua kuwa Stamina amewahi kutangaza kufuata nyayo zake na amekuwa akifanya hivyo kwenye nyimbo zake.

 

 Chid Benz

 

Akizungumzia suala la Chid Beenz rapa huyo ameeleza kuwa bado anaamini uwezo wa Chid Beenz hivyo hakuna sababu ya kumdharau kutokana na kupotea kwake kwenye game, huku akieleza kwa jinsi anavyo amini uwezo wa Chid Beenz hakuna kinacho mshinda kwenye staili ya michano.

 

Chanzo: Mtembezi.com

 

Leave your comment