TANZANIA: “Wasanii wenzangu msiogope kutoa albamu” - Stamina

 

Msanii wa hip hop anayeitambulisha vyema mji usiokuwa na bahari Morogoro, Stamina mesema kuwa hakutoa albamu ya Mt Uluguru ili awe tajiri. Stamina ambaye pia ameshauri wasanii wenzake wasiwe waoga wa kutoa albamu.  Alitamka hayo kwa kusema,”Kusema ukweli mimi mwenyewe ni shuhuda kwenye hilo”.

Stamina aliongeza kwa kusema kuwa,” Yaani wasiogope albamu zinauza japokuwa mimi sikuingiza yangu sokoni ili iwe tajiri, nilitoa ili nijenge heshima yangu. Ili msanii uonekane mkubwa unatakiwa kuwa na albamu”. Mpka  sasa  Stamina ameshauza nakala 850 za albamu ya Mt. Uluguru.

 

Leave your comment