TANZANIA: Mpoki ajiunga na timu E FM Redio!

Mkurugenzi wa E FM, Francis Ciza akimkaribisha Mpoki kwenye timu yao

 

Mchekeshaji maarufu wa Orijino Comedy, Silvester Mjuni anayefahamika kwa jina la Mpoki amejiunga na kituo cha redio cha E FM.

Muigizaji huyo na muimbaji anakuwa miongoni mwa watangazaji wa kipindi cha UBAONI kinachotangazwa na Gadner G. Habash akishirikiana na Bikira Wa Kisukuma (Seth). Kipindi hicho kinaruka hewani kila siku kuanzia saa 9:00 alasiri hadi saa 1:00 jioni.

Kituo hicho cha EFM kilianza kurusha matangazo yake mwaka 2015, na kinazidi kushika kasi kwa matangazo mazuri yaliyochochewa na bipindi vyenye ubunifu ndani yake.Pia kwa kuajiri watangazaji maarufu kama Maulid Kitenge, Dina Marious na wengine wengi, huku nae Mpoki akiongezeka katika timu hiyo.

Leave your comment