Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘I Miss You’ Akimshirikisha Zuchu

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki tajika kutokea nchini Tanzania Rayvanny ameachia ngoma mpya kabisa ya kuitwa ‘I Miss You’ ambayo amemshirikisha Zuchu.

‘I miss You’ ni ngoma ya mapenzi ambayo ndani yake Rayvanny anaonesha majuto yake baada ya kumuacha mpenzi wake kwa hasira. kupitia kibao hiki anamuomba mpenzi wake huyo wa zamani warudiane upya.

Soma Pia: Zuchu Akana Kutumia Maneno Machafu Kwenye Mahojiano

"Hivi bado una hasira bado unanichukia bado una kinyongo. Moyo wako ulishazira bado unaninunia hivi bado una usongo. Kusema bora tuachane ndo kauli inaniuma kila nikikumbuka. Tusitafutane sikujua narusha jiwe ndege ukapepea," anaimba Rayvanny kwenye aya ya kwanza.

Bila shaka hujawahi kumsikia Zuchu akiimba kwa hisia kama alivyofanya kwenye aya ya pili ya kazi hii. Kando na mashahiri ya Zuchu kuashiria kuwa amekataa kata kata msamaha wa Rayvanny, sauti yake inaashiria kuwa hayupo tayari kurudiana na mpenzi wake huyo.

Soma Pia: S2kizzy Atangaza Ujio Wa Albamu Yake Mwaka Huu

"Sipendi tuchukiane japo najua Mungu amenilinda na mengi. Sisemi turudiane ila tambua mimi nilipovunja sijengi," anaimba Zuchu kwenye aya ya pili.

Hii ni ngoma ya tatu kwa Zuchu na Rayvanny kushiriki kwa pamoja, tukianza na ‘Quarantine’ ya Mei 2020 ngoma ambayo pia ilihusisha wasanii wengine wa Wasafi. Baada ya hapo wawili hawa walikutana kwenye ‘My Number One’ kibao ambacho pia kilipokelewa kwa mikoni miwili na mashabiki.

https://www.youtube.com/watch?v=T69CmY6Kc5g

Leave your comment