Producer S2kizzy Aeleza Sababu ya Wasanii Wengi Watanzania Kufanya Amapiano

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji nguli wa muziki kutokea nchini Tanzania S2kizzy hivi karibuni amefichua sababu hasa zinazopelekea wasanii wengi wakubwa kutoka Tanzania kupendelea kufanya muziki wa Amapiano ambao asili yake ni huko Afrika Kusini.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, mtayarishaji huyo wa ngoma ya ‘Tetem’ alitanabaisha kuwa sababu za kibiashara ndio ambazo zimechagiza wasanii wengi kufanya muziki wa Amapiano kwani mashabiki wengi hupendelea muziki wa Amapiano pindi wakiwa sehemu za starehe.

Soma Pia: Marioo Afichua Mchango Wa Wizkid kwenye Tasnia Ya Muziki Nchini Nigeria

"Muziki ni biashara, watu wanaenda club watu wanatoka wanaenda mavidimbwi end of the day miziki inayopigwa ni hiyo (Amapiano). Kwa wasanii pia wanaangalia vitu gani ambavyo wanaweza wakaingia playlist za MaDJ mbalimbali. End of the day this is business. Tunafanya kwa ajili ya biashara tupate pesa" alizungumza S2kizzy.

Kipindi cha hivi karibuni watu wengi maarufu kama Eric Omondi, AY, Maua Sama na wengineo walijitokeza kupinga muziki wa Amapiano kwa kusema kuwa unaua muziki wa Bongo Fleva kitu ambacho S2kizzy amesema si cha kweli kwani hata Amapiano nao ni muziki wa Afrika.

Soma Pia: Marioo Afichua Mchango Wa Wizkid kwenye Tasnia Ya Muziki Nchini Nigeria

"Mimi sikubali kwamba Amapiano inaua muziki fulani. Ile ni culture ya watu fulani South Africa ndio lakini its African music na sisi inabidi tufanye muziki wa kiafrika wowote ule. We are all Africa. We are all one. We can do whatever we want lakini kusema unaua ni hapana," alizungumza S2kizzy.

Nchini Tanzania, S2kizzy ni moja ya watayarishaji wa muziki walioweza kutengeneza ngoma za Amapiano zilizoburudisha masikio ya wasikilizaji ikiwemo ‘Iyo’ ya Diamond Platnumz akimshirikisha Focalistic, Mapara A Jazz na Ntosh Gazz pamoja na’Chawa’ ya kwake Whozu, Rayvanny pamoja na Ntosh Gazzi.

Leave your comment