Zuchu Adokeza Tarehe Atakayoachia Video Ya 'Kitu'

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia wa muziki wa bongo Zuchu amedokeza tarehe ambayo ataachia video rasmi ya wimbo wake mpya uliyopewa jina la 'Kitu'. Kwa mujibu wa chapisho aliloliweka mtandaoni, huenda Zuchu akaachia video ya ngoma hiyo Jumatatu, wiki ijayo.

 "Jumatatu Hii Kuna #KITU," Zuchu aliandika mtandaoni. Aidha, taarifa hiyo ilichapishwa na Wasafi Media.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia ‘Kitu’

Ngoma hiyo kufikia sasa imeachiwa katika mifumo mbili; moja ikiwa audio yake tu, na nyingine ikiwa video yake ya densi.

Kufikia sasa audio ya ngoma hiyo kwenye mtandao wa YouTube imefikisha watazamaji 145,407 huku video yake ya densi ikiwa imetazamwa mara 1,058,012.

Zuchu amewashirikisha wasanii Bontle Smith na Tyler ICU kwenye ngoma hiyo ambayo imepata mapokezi mazuri miongoni mwa mashabiki.

Soma Pia: Nyimbo Tano Zilizofanya Vizuri TikTok Kwa Mwaka 2021

'Kitu' ambayo imeimbwa katika mtindo wa amapiano, iliachiwa mnamo tarehe 22 mwezi Disemba mwaka jana. Ngoma hiyo imeachiwa wakati mtindo wa amapiano umezua mjadala mkubwa.

Hivi maajuzi Zuchu alilazimika kuwatetea wasanii wanaofanya Amapiano, na vile vile kupinga dhana kuwa amapiano imeuua mtindo wa bongo.

 Kwa mujibu wa Zuchu wasanii kufanya muziki wa Amapiano ni jambo zuri kwani inachangamsha tasnia ya muziki kwa kuleta mabadiliko.

 "Bongo flavor can never die artists are going out of their comfort zones its called diversity. Trying new sounds has never killed any industry the music industry is big so let artists try out new things ndo mabadiliko hayo," Zuchu alichapisha kwenye ukurasa wake wa kijamii.

Leave your comment