Jay Melody Aeleza Sababu ya Kuachia Ngoma Yake ya ‘Sugar’ Mwezi Disemba 2021

[Picha: Ghafla]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki na mtunzi mashuhuri kutokea nchini Tanzania Jay Melody amefunguka kuhusu sababu hasa za kuachia ngoma yake ambayo inafanya vizuri kwa sasa ya kuitwa ‘Sugar"’.

Jay Melody aliachia ngoma ya ‘Sugar’ mwishoni kabisa mwa mwezi Desemba ikiwa imetayarishwa na Mocco Genius na ni ngoma ambayo ndani yake Jay Melody anaonesha ni kwa namna gani amezama kimapenzi na mwandani wake huku akimsihi wasiachane.

Soma Pia: Lebo Tano Kutoka Tanzania Zinazotarajiwa Kufanya Vizuri Mwaka 2022

Akiongea kwenye mahojiano aliyoyafanya kwenye kituo cha Times FM, Jay Melody amefunguka kuwa ameachia ngoma hiyo kwa lengo la kusindikiza na kuburudisha watu kipindi cha Valentine na ndio sababu ameiachia mwezi Desemba.

"Target kubwa zaidi nadhani nia yangu ilikuwa ifike mpaka kipindi cha Valentine hii ngoma kwa sababu huu ni mwezi wa kwanza na ngoma imetoka mwezi wa kumi na mbili mwishoni then tunaingia mwezi wa pili hapo mambo ya mapenzi na vitu kama hivyo lakini pia kuwafariji watu kipindi kama hicho, kwa hiyo target yangu kubwa ni kuwafariji watu kipindi cha mapenzi," alizungumza Jay Melody.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video Mpya Ya ‘Rara’

Kupitia ngoma ya ‘Sugar’,  Jay Melody amezidi kudhihirisha kuwa ana uwezo mkubwa wa kuandika ngoma za mapenzi kwani ngoma zake kama ‘Huba Hulu’, ‘Najieka’ na ‘Sambaloketo’ zinazidi kuonesha uwezo wake kwenye eneo hilo.

Leave your comment