Wasanii Kutoka Tanzania Wanaotazamwa Zaidi Kwa Mwaka 2022

[Picha: IPP]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kiwanda cha muziki nchini Tanzania bila shaka kilichangamka na kufanya vizuri mwaka 2021 na hii ni kutokana na wasanii mbalimbali kutoka nchini humo kujituma na kuweka jitihada za ziada kwenye kazi zao.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny na Harmonize Waongoza Orodha ya Wasanii Wenye Wafuatiliaji Wengi Zaidi YouTube Afrika

Safari ya mwaka 2022 ikiwa ndo kwanza imeanza hii hapa ni orodha ya wasanii kutoka nchini Tanzania ambao wanatarajiwa kufanya mambo makubwa zaidi kwa mwaka huu:

Mac Voice

Baada ya kutetemesha nchi na EP yake ya ‘My Voice’, mwishoni mwa mwaka jana, kwa sasa kila mtu anasubiri namna ambavyo msanii huyu kutoka Next Level Music ataupamba mwaka 2022. Kwa Mac Voice, wengi wanatarajia atafanya collabo nyingi zaidi, atashinda na kuteuliwa kwenye tuzo mbalimbali za kimataifa na pengine kutoa albamu yake ya kwanza chini ya Next Level Music.

Soma Pia: Wasanii 5 wa Bongo Wanaotarajiwa Kuachia Albamu Mwaka 2022

Hanstone

Baada ya tetesi kuzagaa mwaka 2021 kuwa Hanstone ameondoka kwenye himaya ya WCB, msanii huyo ambaye aliachia EP yake ya ‘Amaizing’ mwezi Oktoba anatarajiwa kuwasha moto zaidi kunako 2022. Watanzania wengi wanatamani kusikia kazi nyingi zaidi kutoka kwa Hanstone.

Diamond Platnumz

Diamond Platnumz anatarajiwa kuupamba mwaka 2022 na albamu yake mpya ambayo kwa muda sasa imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki nchini Tanzania. Wachambuzi wengi wa muziki wameshuku kuwa albamu hiyo huenda ikawa bora sana kiasi cha kuwania tuzo kubwa duniani kama tuzo za Grammy huko nchini Marekani.

Zuchu

Ikumbukwe kuwa 2021 ni mwaka ambao Zuchu alitoa ngoma nne tu ambazo pamoja na kufanya vizuri, hazikukata kiu ya burudani kwa mashabiki hivyo kwa mwaka huu mzaliwa huyo wa visiwani Zanzibar anatarajiwa kuachia EP au Albamu kabisa ili kukidhi matakwa ya mashabiki.

Rosa Ree

Mwaka huu tutarajie albamu kutoka kwa rapa huyu ambaye alipata uteuzi kwenye tuzo za Afrimma mwaka 2021 kama rapa bora wa kike. Rosa Ree anatarajiwa kuachia kazi zaidi mwaka huu na kuzidi kuuheshimisha muziki wa Hiphop nchini Tanzania.

Leave your comment