Nyimbo Mpya: Ibraah na Harmonize Waachia Video ya 'Addiction'

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii nyota wa bongo fleva Ibraah kwa ushirikiano na Harmonize ameachia video ya wimbo wake mpya uliopewa jina la 'Addiction'.

Kwenye ngoma hiyo, wasanii hao wawili wanasifu pombe na kusimulia madhara pamoja na hali mbali mbali ambayo hutokana na kunywa pombe. Ibraah ndiye anayefungua wimbo huo kwa sauti yake laini.

Soma Pia: Nyimbo Tano Zilizofanya Vizuri TikTok Kwa Mwaka 2021

"Kwanza pombe ni dawa, ukiwa na msongo wa mawazo inakueka sawa, pombe sio kahawa, kama huwezi usizidishe ukapagawa, mwenzenu nikinywaa pombe, zinashuka za chini na kichwa kinakuanga cha moto, Na Sio Za Kupimaa Pomba Iwo Dompo Iwe Bariml Zinanishikaga Nolo Changamoto, na Enjoy Japo Nikinywa Nakunja sura ni moja ya utamu wa pombe. Sitoboi sasa usiombe niikamate chura Nazima taa hiki kikombe," Ibraah anaimba katika mwanzo wa wimbo.

Soma Pia: Bifu Tano Kubwa Kwenye Bongo Fleva Mwaka 2021

Mdundo wa ngoma hii ni wa amapiano na umetayarishwa na Moco Genius ambaye anafahamika kwa kufanya kazi na wasanii wakubwa nchini Tanzania.

 

Video ya wimbo huu imeelekezwa na Director Chris chini ya kampuni ya Redshot production. Wahusika kwenye video hii wapo katika mandhari ya watu ambao wanajiburudisha kwa pombe na kusakata densi pia.

 

Aidha, wachekeshaji maarufu nchini Tanzania Masele na Kobele wamehusika kwenye video hiyo na imefurahisha wengi. Video ya 'Addiction' imepata mapokezi mazuri mno na tayari ishatazamwa na maelfu ya mashabiki mtandaoni.

https://www.youtube.com/watch?v=aDH9It7oD-A

Leave your comment