Ibraah Amshukuru Harmonize Kwa Kumsaidia Kufanikisha Tamasha la Ibraah Homecoming

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki wa kizazi kipya Ibraah amemshukuru bosi wake Harmonize kwa kuchangia katika mafanikio ya tamasha lake la Ibraah Homecoming lililofanyika uwanja wa Nangwanda mkoani Mtwara.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Ibraah alisema kuwa uwepo wa Harmonize kwenye tamasha hilo ulikuwa na maana kubwa kwake.

Soma Pia: Ibraah Apata Mafanikio Makubwa Katika Tamasha Lake la Ibraah Homecoming

Alifichua kuwa hakuwa na uhakika iwapo Harmonize atatumbuiza kwenye onyesho hilo na hivyo basi ujio wake ulimfurahisha mno.

"What a surprise thank you so much bro, sikutegemea kama utaungana namimi kwenye siku yangu kubwa nyumbani mtwara!! God bless you bro," chapisho la Ibraah kwenye ukurasa wake wa Instagram lilisomeka.

Harmonize, kando na kuhudhuria tamasha la Ibraah Homecoming, alipanda jukwaani na kuwaburudisha mashabiki kwa ngoma zake kali.

Soma Pia: Ibraah Azungumzia Utata Uliotokea Konde Music Worldwide Kabla ya ‘Jipinde’ Kuachiwa

Burudani ilizidi na hata kwa wakati mmoja Harmonize aliwapandisha mamake pamoja na mpenziwe jukwaani. Ikumbukwe kuwa Harmonize na Ibraah wameshirikiana kwa ngoma kadhaa ambazo zilifanya vizuri sana.

Wawili hao walitumbuiza ngoma hizo kwa pamoja huku mashabiki wakionekana kuwa wachangamfu mno. Wasanii wengine kutoka lebo ya Konde Music Worldwide alikosainiwa Ibraah pia walitumbuiza kwenye tamasha hilo.

Tamasha la Ibraah Homecoming lilipata mafanikio makubwa haswaa ikizingatiwa kuwa Ibraah hajakuwepo kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu sana. Uwanja wa Nangwanda ulijaa pomoni huku mauzo ya tiketi yakiendelea hadi usiku.  

Leave your comment