Ibraah Apata Mafanikio Makubwa Katika Tamasha Lake la Ibraah Homecoming

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Ibraah ameandikisha historia katika muziki wake baada ya kujaza uwanja wa Nangwanda mkoani Mtwara kupitia tamasha lake la Ibraah Homecoming.

Ibraah Homecoming ndilo lilikua tamasha la kwanza la Ibraah kama msanii. Tamasha hili pia lilikuwa njia ya Ibraah kuwashukuru mashabiki wake wa nyumbani ambao wamemuunga mkono tangu akiwa mchanga kwenye tasnia ya muziki.

Soma pia: Anjella Atangaza Ujio wa EP Yake ya Kwanza Tangu Aanze Muziki

Uwanja wa Nangwanda ulijaa pomoni hadi kutapika, hili lilikuwa dhihirisho tosha kuwa mcheza kwao hutuzwa. Wasanii tajika walipanda jukwaani mmoja baada ya mwingine na kutumbuiza mashabiki ambao kwa kweli walionekana wachangamfu mno.

Baadhi ya wasanii waliokuwepo kwenye tamasha hilo ni Barnaba Classic, H Baba, Amber Lulu, Countrywizzy, Anjella na wasanii wengine wengi ikiwemo bosi wake Ibraah Harmonize ambaye aliambatana na mamake pamoja na mpenziwe.

Mafanikio ya tamasha hilo yamemfanya Ibraah kuwa gumzo miongoni mwa wadau mbali mbali kwenye tasnia ya muziki. Wengi walimpongeza kwa mafanikio hayo na kumtakia mema kwenye safari yake ya muziki.

Ibraah kwa sasa amedhihirisha kuwa amepanda ngazi na yeye sio msanii chipukizi tu bali msanii mwenye ushawishi mkubwa kwenye tasnia ya muziki wa bongo.

Soma Pia: Ibraah Aachia Ngoma Mpya ‘Addiction’ Akimshirikisha Harmonize

Hapo awali Ibraah alipamba vichwa vya habari baada ya kujiandikishia historia kupitia ngoma yake ya 'Jipinde' ambayo ilipata idadi ya watazamaji wengi mno ndani ya muda mfupi.

Leave your comment