Rais Samia Awafurahisha Watanzania Baada ya Kutaja Marioo, Harmonize Kwenye Hotuba Yake

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu amewavunja mbavu watanzania kutokana na kauli aliyotoa kwenye hotuba yake kuhusu wasanii Marioo na Harmonize.

Rais Samia alitoa kauli yake kuhusu wasanii hao wawili ambao walitumbuiza katika hafla aliyohudhuria.

Soma Pia: Anjella Atangaza Ujio wa EP Yake ya Kwanza Tangu Aanze Muziki

Punde tu baada ya wasanii hao kuondoka jukwaani, Rais Samia aliingia na kuanza kwa kupongeza vikundi tofauti vya burudani vilivyotumbuiza kwenye hafla hiyo. Alianza kwa kumpongeza Marioo na kutoa kauli yake kuhusu ngoma yake mpya ambayo imepewa jina la 'Beer Tamu'.

Wimbo huu ambao kufikia sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni mbili kwenye mtandao wa YouTube umempa Marioo mafanikio makubwa.

Rais Samia alisema kuwa ni jambo la kufurahisha kuwa licha ya Marioo kuimba wimbo unaosifu vileo, yeye mwenyewe hanywi vileo hivyo.

Soma Pia: Rayvanny Adokeza Ujio wa Kolabo Baina Yake na Justin Bieber

"Lakini tumemsikia Marioo. Ingawa Marioo anawaambia wenzio ule unywaji ni mtamu lakini yeye hanywi. Kwa hiyo muangalie vizuri hapa, anayekupa message akakisifia kitu na yeye hafanyi. Kama yeye hafanyi muulizeni kwanza kwa nini," Rais Samia alisema.

Vile vile alimpongeza Harmonize huku akimtaja kwa kutumia jina lake la usanii la Tembo. Alisema kuwa kwa kweli muonekano wa Harmonize unafaa jina hilo la Tembo.

 "Lakini pia nimemwona Konde Boy, Tembo na kwa kifua kile kweli ni tembo," Rais Samia aliongezea.

Waliohudhuria hafla hiyo walibaki wamecheka kutokana na kauli ya Rais Samia. Rais Samia amepongezwa na wengi kutokana na mchango wake kwenye ukuaji wa tasnia ya muziki wa Tanzania.

Leave your comment