Harmonize na Anjella Washirikishwa Kwenye Albamu Mpya ya DJ Neptune

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji maarufu wa muziki kutoka Nigeria DJ Neptune ameachia orodha ya nyimbo zilizoko kwenye albamu yake ijayo.

Japo DJ Neptune sio mwimbaji, yeye huunganisha wasanii mbali mbali kutoka bara la Afrika kwenye albamu zake.

Soma Pia: Ibraah Aachia Ngoma Mpya ‘Addiction’ Akimshirikisha Harmonize

Anachokifanya ni kuwa anatengeneza midundo ya nyimbo na kisha kuwaleta pamoja na kuwashirikisha wasanii mbali mbali kutoka bara la Afrika, kisha mwisho wa siku kumiliki ngoma yote.

Kwenye albamu yake ya pili iliyopewa jina la 'Greatness 2.0' ambayo inatoka mnamo tarehe 26 mwezi huu wa Novemba, ni wasanii wawili tu kutoka Afrika Mashariki ambao wamehushiwa mle ndani.

Soma Pia: MB Dogg Asimulia Masaibu Aliyopitia Katika Muziki

Wasanii hao wawili ni pamoja na msanii nyota wa muziki wa bongo Harmonize na malkia mwenye sauti ya kuvutia mno Anjella.

Majina ya wasanii hao wawili kutokea kwenye albamu hiyo ina maana kubwa sana kwani albamu hiyo vile vile imewahusha wasanii wakubwa wa Afrika ikiwemo Omah Lay, Adenkule Gold, Yemi Alade, Simi, Patoranking, Rema, Focalistic, Joeboy na wengine wengi.

Ngoma ambayo imewaleta Harmonize na Anjella pamoja kwenye albamu hiyo imepewa jina la 'My Woman' na inatarajiwa kuwa na utofauti mkubwa na kazi zao za hapo awali kwani mara hii waliohusika kwenye utengenezaji ni watu wapya ambao pia ni mastaa wa kimataifa.

Hii si mara ya kwanza Anjella na Harmonize kushirikiana, wawili hao pia walitoa ngoma kama vile 'One time', 'All night', 'What Do You Miss' na 'Kama'.

Leave your comment