Harmonize Akataa Kulinganishwa na Msanii Yeyote, Aapa Kuibadilisha Tasnia ya Muziki

[Picha: The Standard]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki barani Afrika Harmonize amejitokeza na kujipiga kifua kwa kuwa msanii bora ambaye atabadilisha tasnia ya muziki.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Harmonize vile vile alikataa kulinganishwa na msanii yeyote.

Soma Pia: Rayvanny Aweka Rekodi Baada ya Kutumbuiza Kwenye Tuzo za MTV EMA

Nyota huyo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide, alisema kuwa ni makosa sana kumlinganisha na msanii yeyote kwani yeye ako na sauti bora zaidi.

Harmonize kwenye chapisho hilo mtandaoni alisema kuwa lengo lake kuu ni kuimba nyimbo ambazo zitaburudisha kizazi kipya, na hivyo basi mashabiki ambao kidogo umri wao umezidi hawataelewa nyimbo zake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Linex Aachia EP Mpya ‘Tatu za Mjeda’

Alisema kuwa iwapo mtu atasikiliza albamu yake ya ‘High School’ kwa makini, basi atagundua sababu ya yeye kusema kuwa anafanya muziki tofauti.

"You're so wrong if you compare me with any artist in the game cuz I sound better than anyone you know, I'm going to change this game just a matter of time if you listen to #highschool I hope you know what I'm talking about im doing this or new generation ony hama ushazeheka yani us apitwa na wwi you can't love my music yani kama una miaka kuanzia 50 you can't understand my sound pop," ujumbe wa Harmonize mtandaoni ulisomeka.

Ujumbe huu unatokea muda mfupi baada ya yeye kuachia albamu ya "High School" ambayo imekuwa ikilinganishwa na albamu ya "Only One King" kutoka kwa Alikiba.

Albamu hizo mbili zilitoka katika kipindi kimoja huku zikiachania siku chache sana. Alikiba ndiye alikuwa wa kwanza kuachia albamu yake kabla ya Harmonize kufuata.

Leave your comment