Dullah Planet Ataja Wasanii 3 wa Bongo Ambao ni Wazuri Zaidi Kufanya Mahojiano Nao

[Picha: East Africa TV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtangazaji maarufu kutokea nchini Tanzania Dullah Planet, ambaye anatangaza kipindi cha muziki cha Planet Bongo, amewataja wasanii watatu wakali ambao humfurahisha na hujibu maswali kwa ufasaha sana kwenye mahojiano.

Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu ya Kuita Albamu Yake ‘Only One King’

Akiongea kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha Times FM, Dullah Planet ambaye pia ni muigizaji alidokeza kuwa hufurahi sana kufanya mahojiano na rapa Professor Jay kutokana na uwezo wake mkubwa wa kujibu maswali.

"Profesa Jay atachukua namba moja, nimefanya nae interviews nyingi na kati ya zote nimejifunza na nimeenjoy, kwa sababu anajibu maswali kwa uzoefu yaani ukimuuliza kitu fulani atakupa mfano kuna wakati ilikuwa hivi na hivi kikatokea kitu Fulani," alizungumza Dullah Planet.

Soma Pia: Alikiba Azungumzia Killy na Cheed Kuondoka Kings Music

Pia Dullah Planet alimtaja Juma Nature pamoja na Chid Benz kama wasanii ambao wanajibu maswali kwa weledi pale anapofanya nao mahojiano.

"Juma Kassim Kiroboto (Juma Nature) yeye kwa sababu ya mswahili atafupisha jibu lakini haachi comedy lazima atakuachia neno ambalo litakuchichibua kidogo. Rashid Abdallah Makwiru Chid Benz kwanza atakuudhi alafu utafurahi sana, mwanangu kabisa kutoka Ilala," Dullah Planet alizungumza.

Dullah ni mtangazaji wa kipindi cha burudani cha Planet Bongo kinachoruka kwenye East Africa Radio kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa.

Dullah ni mojawapo ya watangazaji wanaoheshimika sana kwenye kiwanda cha Bongo Fleva kwani ana uzoefu mkubwa wa zaidi ya miaka 10 kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Kufikia sasa, ameshafanya mahojiano na wasanii wakubwa nchini Tanzania kama vile Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Ibraah, Harmonize, Rayvanny, Darassa, Marioo na wengineo wengi.

Leave your comment