Ibraah Afichua Sababu ya Kumwacha Harmonize Marekani na Kurudi Tanzania

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Ibraah ameibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki baada ya kumwacha bosi wake Harmonize Marekani na kurejea Tanzania. Harmonize na Ibraah hapo awali waliondoka Tanzania na kuelekea Marekani kwa ziara ya muziki ambaye iliratibiwa kudumu kwa miezi miwili.

Wengi wa mashabiki walitarajia kuwa Ibraah angebaki Marekani kwa muda huo hadi Harmonize atakapo kamilisha ziara yake. Akizungumza baada ya kutua Tanzania, Ibraah alifafanua kuwa yeye alikuwa amemaliza shughuli yake kwenye ziara ya Harmonize na hivyo basi alirejea nyumbani kuwatumbuiza mashabiki wake.

Soma Pia: Ibraah Azungumzia Ziara ya Muziki ya Harmonize Kulinganishwa na Ile ya Diamond

 Alieleza kuwa aliratibiwa kutumbuiza katika onyesho mbili kwenye ziara hiyo na baada ya kumaliza, aliitwa nyumbani Tanzania ambako pia anafaa kutumbuiza katika onyesho lake.

"Mimi nilikuwa na show zangu na show zangu nilizoenda kufanya kule nishamaliza. Kwa hivyo nimekuja kufanya show zangu ambazo ni za watu wangu wa nyumbani, watu wangu wa fujo, ndio nimerudi ndio nimerudi," Ibraah alisema wakati anahojiwa na wanahabari.

Soma Pia: Maud Elka Aashiria Uwezekano wa Kolabo Baina yake na Ibraah, Diamond

Msanii huyo aliongezea kuwa alijifunza mengi katika taaluma yake ya muziki kipindi ako kwenye ziara ya Harmonize. Aidha, alisemaa hali kwenye tasnia ya burudani Tanzania ni tofauti kidogo na alikuwa ametamani sana kurudi nyumbani kwa mashabiki wake.

Ibraah ni mmoja wa wasanii kutoka lebo ya Konde Music Worldwide wanaofanya vizuri sana. Kabla kuondoka kwenda Marekani, aliachia wimbo wa 'Jipinde' ambao umetazamwa takriban mara milioni tatu nukta tano kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment