Zuchu Alalamika Makampuni Kutowalipa Wasanii

[Picha: TMZ KE]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki Zuchu kutoka lebo ya WCB amelalamika mtandaoni baada ya kukosa kulipwa na kampuni aliyoifanyia ubalozi.

Zuchu alichapisha ujumbe mrefu ambao alieleza jinsi baadhi ya makampuni hupuuza wasanii na kukataa kuwalipa licha ya wao kuweka bidii katika kazi yao.

Soma Pia: Wasifu wa Rosa Ree, Safari Yake Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Mahusiano na Thamani Yake

Zuchu alidai kuwa ni jambo la kusikitisha wakati kampuni inakosa kutii makubaliano ambayo wako nayo na msanii. Aliongeza kuwa hii ndio kazi ya wasanii na inafaa kuheshimiwa.

"Am so disappointed with some of these people we work with ifikie muda msanii aheshimiwe kwa status na platform yake inayotumika kutangazia kitu flani .Hii sio favor wala 510 msaada tunafanya kazi kwa makubaliano basi ifikie hatua mujifunze kuheshimu wasanii," Zuchu aliandika.

Soma Pia: Wasifu wa Anjella, Safari Yake Kimuziki, Nyimbo Zake Bora, Mafanikio, Mahusiano na Thamani Yake

Kwa mujibu wa Zuchu, wasanii wa kike wamepuuzwa sana na juhudi zao huambulia patupu mara kwa mara.

"Na kinachonikera zaidi ni kwamba wanajua umefanya kazi kubwa kushikilia bango kwa kiasi kikubwa kuchangia ushawishi kwenye matumizi ya kampuni zao .Watu wengi/makampuni sometimes munadharau sana wanawake kwenye upande wa malipo respect a woman who has worked," msanii huyo aliongezea.

Maneno ya Zuchu yamebeba uzito mwingi na yameibua hisia mtandaoni haswaa ikizingatiwa kuwa yeye ni mmoja wa wasanii wa kike wanaoheshimika sana na wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.

Zuchu hata hivyo hakufichua jina la kampuni ambalo lilikuwa limekosa kumlipa.

Leave your comment