Jux, Nandy Waashiria Ujio wa Kolabo na Patoranking

[Picha: Jux Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu kutoka nchini Nigeria Patoranking hivi maajuzi alitua Tanzania kwa shughuli nzima ya kutii mwaliko wa uzinduzi wa albamu ya Alikiba ya 'Only One King'.

Alikiba na Patoranking wameshirikiana katika wimbo wa ‘Bwana Mdogo’ ambao pia unapatikana kwenye albamu hiyo. Patoranking hata hivyo pia alikua na shughuli zingine za muziki kando na kukutana na Alikiba.

Soma Pia: Harmonize Apendezwa na Album Mpya ya Alikiba 'Only One King'

Kufikia sasa, baadhi ya wasanii wa bongo washadokeza ujio wa kolabo baina yao na Patoranking. Staa wa muziki Jux alidhibithsa kuwa yumo jikoni pamoja na Patoranking na hivi karibuni atawapakulia mashabiki wake wimbo mtamu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jux alichapisha picha iliyomwonyesha akiwa pamoja na Patoranking na mtayarishaji wa muziki S2kizzy wakirekodi wimbo.

Kando ya picha hiyo, Jux aliandika ujumbe ambao ulidhibitisha kuwa ni rasmi kolabo baina yake na Patoranking ipo njiani. "@s2kizzy on the beat you already know is a hit @patorankingfire #KingOfHearts @africanboy_brand," Jux aliandika mtandaoni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Alikiba Hatimaye Aachia ‘Only One King’ Album

Msanii mwingine wa bongo ambaye amedhibitisha kolabo na Patoranking ni Nandy. Malkia wa bongo alichapisha picha ambazo vile vile zilimwonyesha studioni na Patoranking wakirekodi wimbo.

Patoranking ni msanii ambaye amekuwa wazi kufanya kazi na wasanii wa bongo. Hapo nyuma aliwahi fanya kolabo na msanii Rich Mavoko na pia Diamond Platnumz kwenye wimbo wa 'Love You Die'.

Wimbo wa 'Love You Die' ulivuma sana na kupata takriban watazamaji milioni hamsini na tatu kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment