Nandy, Patoranking Waingia Studio Nchini Zanzibar

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bingwa wa muziki kutoka Tanzania Nandy ameendelea kupiga hatua kwenye muziki wake baada ya kuonekana akiwa studio na nyota kutokea nchini Nigeria Patoranking ambaye kwa sasa yupo Tanzania.

Nandy alichapisha picha kwenye akaunti yake ya Instagram ambapo alionekana akiwa na Patoranking studio huko visiwani Zanzibar.

Soma Pia: Nandy Na Mr Eazi Waashiria Ujio Wa Kazi Yao Mpya

"Work till last breathe…..my broda Patoranking," aliandika Nandy.

Patoranking ni msanii kutokea Nigeria mwenye heshima kubwa barani Afrika kwani kufikia sasa ameshatoa ngoma ambazo zimetikisa Afrika nzima kama vile ‘Girlie O’, ‘My Woman’ pamoja na ‘Suh Different’.

Kwa sasa, Patoranking yuko nchini Tanzania ambapo msanii huyo alipokelewa na Alikiba huko Zanzibar wiki iliyopita na wengi wameshuku kuwa wawili hao yaani wako katika harakati za kutengeneza video ya ngoma ambayo wamefanya pamoja.

Soma Pia: Kolabo Tano Kali Zilizohusisha Wasanii wa Tanzania na Kenya

Kazi hii ya Nandy na Patoranking kama itaingia sokoni itaendeleza utamaduni wa wasanii mbalimbali watanzania kufanya kazi na msanii Patoranking, kwani Rich Mavoko alishirikiana na Patoranking kwenye ‘Rudi’, Navy Kenzo walishirikiana naye kwenye ‘Bajaj’, kisha Diamond Platnumz akazidi kukoleza utamaduni huo kwenye ‘Love You Die’ mwaka 2017.

Kwa upande wa Nandy, ameendelea kuupeleka muziki wake kwenye medani za kimataifa baada ya siku mbili zilizopita kuachia ‘Usinimwage’ ngoma ambayo ameshirikishwa na nyota kutokea Kenya Arrow Bwoy.

Leave your comment