Cheed Atangaza Tarehe Atakayoachia Ngoma Yake Ya Kwanza Chini Ya Konde Music Worldwide

[Picha: Killy Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii chipukizi Cheed ametangaza tarehe kamili ambayo ataachia kazi yake ya kwanza chini ya usimamizi wa lebo ya Konde Music Worldwide. Cheed hapo awali alikua amesainiwa katika lebo ya Kings Music kabla ya kuhama na kuenda Konde Music Worldwide pamoja na mwenzake Killy. 

Soma pia: Nandy Na Mr Eazi Waashiria Ujio Wa Kazi Yao Mpya

Cheed na Killy walitambulishwa rasmi kama wanachama wa Konde Music Worldwide mwaka jana. Japo Killy aliweza kutoa ngoma na hata kupata umaarufu, Cheed alisalia kimya. Ukimya wa Cheed katika lebo ya Konde Music uliibua maswali mengi miongoni mwa wadau mbali mbali. Katika mahojiano ya hivi karibuni, msanii Anjella kutoka lebo hiyo hiyo aliulizwa na wanahabari sababu ya Cheed kuchelewa kutoka ila hakuwa na jibu kamili. 

Katika tangazo la hivi karibuni, Cheed ametangaza kuwa kazi yake ya kwanza itatoke tarehe 24 mwezi huu. Aliambatanisha tangazo hilo na simulizi ya maisha yake na changamoto alizopitia katika safari yake ya muziki. 

. "Kila Kijana Ana Ndoto Lakini ili Utimize Ndoto hizo ni Lazima Uwe Mvumilivu,Msikivu na Mwenye Kusubiri Wakati Wa Mungu,Nimepitia Mengi Kwenye Safari Yangu Ya Muziki Lakini Naamini Safari Hii Ndio Safari Sahihi Na Muda Sahihi Wa Mungu,Ahsante Mashabiki Zangu kwa Kunivumilia Na Kunisubiri Kwa Kipindi Chote! Sasa Nakuja tena Tar 24 September 2021. Naombeni Support yenu kwani bila Ninyi Hakuna Cheed," Chapisho la Cheed lilisomeka.

Leave your comment