Msanii Mpya Wa Rayvanny Kuachia Ngoma Yake Siku Moja Na Wa Harmonize

[Picha: Instagram ]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii tajika Rayvanny na Harmonize wamezua gumzo mitandaoni kutokana na matangazo ambayo lebo wanazomiliki wameachia hivi karibuni. Rayvanny anamiliki lebo ya Next Level Music ambayo imemtambulisha msanii wake wa kwanza ambaye ni Mac Voice. Harmonize kwa upande mwingine anamiliki lebo ya Konde Music Worldwide ambayo vile vile inatarajia kumtoa msanii wao mpya kwa jina la Cheed. 

Soma pia: Chege Aeleza Sababu Ya Kuepuka Kufanya Muziki Wa Amapiano

Kilichoibua maswali miongoni mwa mashabiki na wadau tofauti ni kuwa Mac Voice na Cheed wataachia ngoma zao za kwanza chini ya lebo hizo tarehe 24 mwezi huu. 

Hii imeonekana kuzidi sadfa kwani wasanii hao wawili wanatoka katika lebo ambazo zinashindana na zinamilikiwa na wasanii ambao wako na tofauti za kibinafsi. Bila shaka macho yote yatakuwa kwa wasanii hao wawili na ngoma ambazo wataachia siku hyo ya Ijumaa. 

Mashabiki wengi watataka kuona ni nani ambaye atatoa ngoma ambayo itapokelewa vizuri. Aidha, Mac Voice amekaribishwa katika familia ya Wasafi na wasanii waliosainiwa chini ya lebo hiyo ikiwemo Zuchu. Kwa upande mwingine Cheed pia amekaribishwa Konde Gang na wasanii wa hiyo lebo ikiwemo Anjella na Ibraah. 

Kabla ya kujiunga na lebo ya Konde Music, Cheed alikuwa amesainiwa katika lebo ya Kings Music inayomilikiwa na Alikiba. Mac Voice kwa upande mwingine kabla ya kuingia Next Level Music alikuwa akijitahidi kutoa ngoma kama msanii wa kujisimamia.

Leave your comment