Nandy Azungumzia Mchango wa Billnass Kwenye Taaluma Yake ya Muziki

[Picha: Classic 105]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Malkia wa muziki wa bongo Nandy amefunguka kuhusu mchango wa mwanamuziki Billnass katika taaluma yake ya muziki. Inaripotiwa kuwa Nandy na Billnass walikua na mahusiano ya kimapenzi ila wakaachana.

Hata baada ya kuachana na kudhihirisha wazi katika mitandao ya kijamii, tetesi ziliibuka mitandaoni kuashiria kuwa huenda wawili hao bado walikua pamoja.

Soma Pia: Zuchu Amsifia Nandy, Adokeza Kuwa Hana Tatizo Kufanya Kolabo Naye

Nandy hata hivyo aliwashangaza wengi hivi maajuzi alipomleta Billnass jukwaani wakati wa tamasha lake la Nandy festival lililofanyika mkoani Dar es Salaam.

Wengi hawakutarajia kuwa wawili hao watakua na ukaribu wa hali hiyo haswaa baada ya penzi lao kuvunjika.

Akizungumza na wanahabari, Nandy amesifia mchango wa Billnass katika maisha yake haswaa taaluma yake ya muziki. Alisema kuwa Billnass ako na mchango wa asilimia kubwa sana katika muziki wake.

Soma Pia: Nandy Amsifia Rais Samia Suluhu Kwa Kukuza Sanaa ya Muziki Tanzania

Aidha, Nandy hakuonyesha uwepo wa tofauti au uhasama wa aina yoyote baina yake na Billnass.

"Billnass ananifanyia vitu vya kipekee kila siku, ni mtu ambaye huwa ananishauri sana. Anamchango mkubwa asilimia hamsini (50%) kwenye mafanikio yangu haya unayoyaona," Nandy alisema.

Wawili hao washawahi kushirikiana katika nyimbo kadhaa zikiwemo 'Do Me' na 'Bugana' ambazo zilipokelewa vizuri sana na mashabiki. Wimbo wa 'Do Me' kufikia sasa umetazamwa takriban mara milioni tatu nukta mbili huku 'Bugana' ukiwa na na watazamaji milioni tatu.

Leave your comment