Diamond Atangaza Tarehe Atakayoanza Ziara yake Marekani

[Picha: Diamond Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Diamond Platnumz kwa sasa yumo mbioni kufanikisha ziara yake ya muziki ya Marekani.

Diamond ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya WCB anatarajiwa kuanza ziara hiyo mnamo tarehe nane mwezi ujao katika mkoa wa Atlanta.

Soma Pia: Zuchu Azungumzia Uhusiano wake wa Karibu na Maproducer S2kizzy na Ayo Lizer

Diamond kupitia chapisho aliloliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram ameonekana kukamilisha tamasha zake za nyumbani na hivyo basi kujiandaa kuwaburudisha mashabiki wake walioko Marekani.

Kwenye chapisho hilo, Diamond aliwaambia mashabiki wake walioko katika mikoa ya Atlanta na Washingtone kujitayarisha kwani atakua anatua huko tarehe nane na kumi.

"Dodoma was a Movie yesterday!!!... Atlanta!! see you Oct 8th , Washington Dc Oct 10th for my DiamondPlatnumzUSATour2021," chapisho la Diamond mtandaoni lilisomeka.

Soma Pia: Diamond ‘Naanzaje’, Jux ‘Sina Neno’, Harmonize ‘Teacher’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii

Diamond aliandika ujumbe huo baada ya kutumbuiza katika hafla ya Mkakati wa Uelemishaji na Uhamasishaji wa Sensaya Watu na Makazi 2022. Kwenye hafla hiyo vile vile kulikuwepo na wasanii wengine wakubwa ikiwemo mshindani wake wa jadi Alikiba.

Kwenye ziara yake Marekani, Diamond atatumbuiza katika mikoa kumi na moja. Ziara yake itakamilika tarehe 31 mwezi Oktoba mkoani Dallas.

Wakati Diamond anajiandaa kuanza Ziara yake, tayari msanii mwenzake Harmonize anaendelea na ziara yake ya muziki huko Marekani. Harmonize aliandamana pamoja na msanii Ibraah kwa ziara hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi miwili. Wasanii hao pia wanatarajiwa kujihusisha na masuala mengine ya kimuziki ikiwemo utayarishaji wa albamu zao.

Leave your comment