Collabo 5 Kali Baina ya Wasanii wa Tanzania na Uganda [Video]

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ni jambo lililo wazi kuwa Tanzania na Uganda ni nchi ambazo zina historia ndefu sana pamoja na urafiki ulioshiba. Uhusiano baina ya nchi hizi mbili umejengeka pia kwenye sekta ya muziki ambapo wasanii wa Tanzania na Uganda wamekuwa wakishirikiana kufanya nyimbo za pamoja.

Soma Pia: Harmonize Adai Muziki wa Kiafrika Utatawala Ulimwengu Mzima

Makala hii inaangazia nyimbo tano ambazo wasanii kutokea nchini Tanzania na Uganda wameimba kwa pamoja:

Pull Up - Eddy Kenzo ft Harmonize

 Ilipofika Julai 2019 Eddy Kenzo aliamua kumshirikisha Harmonize kwenye wimbo wa ‘Pull Up’. ‘Pull Up’ ni wimbo wenye vionjo vya dancehall na uliopambwa na mdundo wenye nguvu kutoka kwa mtayarishaji wa muziki Kuseim Notes. Bila shaka utakufanya ucheze dansi mwanzo hadi mwisho. Kufikia sasa, wibo huu umeshatazamwa mara Laki mbili kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=-pPlhYtV4B0

Yes - Mbosso ft Spice Diana

Wimbo namba 11 kutoka kwenye albamu yake ya ‘Definition of Love’, mwanamuziki Mbosso alimpa shavu mwanadada Spicy Diana kutokea Uganda. ‘Yes’ ni wimbo ambao unafaa sana kwenye sherehe za harusi kutokana na kuwa na mashairi yaliyotulia na kufumwa na maneno ya mahaba. Trone ambaye ndiye mtayarishaji wa wimbo huo alisuka mdundo wa ngoma hii na ala za muziki kama gitaa.

https://www.youtube.com/watch?v=NClIIN8FgF4

 Ndivyo Sivyo - Profesa Jay ft Chameleone

‘Ndivyo Sivyo’ ni wimbo ambao umetoka takriban miaka 13 nyuma lakini mpaka leo ni mojawapo kati ya collabo bora ambazo zimeshawahi kutokea hapa Afrika Mashariki. Tofauti na nyimbo nyingi ambazo zimejikita sana kwenye mapenzi, ‘Ndivyo Sivyo’ ni wimbo ambao unatoa mafundisho ya kimaisha ambapo wasanii hao wamegusia masuala kama kudharau watu, umakini kwenye maisha na mambo mengine mengi.

https://www.youtube.com/watch?v=UWdGA2A0CuE

Mwaga - Fik Fameica ft Rayvanny

Rapa kutokea nchini Uganda Fik Fameica aliamua kuchungulia kiwanda cha muziki nchini Tanzania Novemba mwaka 2018 kumshirikisha Rayvanny kwenye ‘Mwaga’. Kama unatafuta wimbo ambao utakuweka kwenye mood ya kucheza na kufurahi basi "Mwaga" ni kwa ajili yako. Kufikia sasa, video ya wimbo huu imeshatazamwa mara Milioni 1.2 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=WKT5NefqgRg

Kokonya - Spice Diana ft Harmonize

Spice Diana aliamua kuchachua kiwanda cha muziki Afrika Mashariki baada ya kumshirikisha Harmonize kwenye ‘Kokonya’. Ndani ya ngoma hii ambayo imetayarishwa na Nessim pamoja na Daddy Andre, Harmonize ameimba kwa lugha ya kiganda pamoja na kiingereza. Video hii imefanyika hapa Dar Es Salaam chini ya Director Hanscana na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 2.7 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=qc0TyBUdGlk

Leave your comment