Chidi Benz Adai Kuna Uhasama Baina ya Tunda Man na Diamond Platnumz

[Picha: Tunda Man Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki tajika nchini Tanzania Chidi Benz ambaye ni mmoja wa wasanii wakongwe sana Bongo amefunguka na kudai kuwa kuna uhasama baina ya wasanii Tunda Man na Diamond Platnumz.

Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha redio cha Wasafi FM, Chidi Benz alidai kuwa uhasama baina ya wanamuziki hao wawili ndio mojawapo ya uhasama za ukweli.

Soma Pia: Mkubwa Fella Afunguka Kuhusu Bendi Mpya ya New Yamoto Band

Chidi Benz hata hivyo hakueleza kwa kina haswaa chanzo cha tofauti za Tunda Man na Diamond.

"Bifu ya ukweli kabisa, ya ukweli, Tunda ule wa mwili natamani, na Nasibu ndio walikuwa na matatizo ya ukweli kabisa. Kwa sababu umeuliza hilo, kwa taarifa yenu Nasibu na bwana Tunda Man ndio wako na bifu ya ukweli kabisa," Chidi Benz alisema.

Chidi Benz na Tunda Man walikua na ukaribu mno kimuziki katika enzi za bongo flava ya kale.

Soma Pia: Hanscana Ajibu Madai ya Kuchukua Nafasi ya Kenny Pale Zoom Extra

Wawili hao walishirikiana katika wimbo wa ‘Neilah’ ambao kwa wakati huo ulipendwa sana. Tunda Man kwa upande mwingine ni rafiki wa karibu wa msanii Alikiba ambaye pia anadaiwa kuwa na utofauti na Diamond Platnumz.

Hivi majuzi, Tunda Man aliibua gumzo mtandaoni baada ya kuchapisha video ya kitambo iliyomwonyesha yeye pamoja na Alikiba na Diamond. Kwenye ujumbe alioambatanisha na video hiyo, Tunda Man alimshukuru Alikiba kwa kusimama naye katika saana ya muziki licha ya yeye kupitia changamoto chungu mzima.

Leave your comment