Young Lunya Athibitisha Uwepo wa Mimi Mars Kwenye Albamu Yake

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Young Lunya amethibitisha kuwa mwanamuziki mwenye sauti ya kipekee kutokea Mdee Music Mimi Mars atakuwepo kwenye albamu yake inayotarajiwa kuachiwa mwaka huu.

Lunya ambaye yuko chini ya Intersource Records kupitia akaunti yake ya Instagram sehemu ya Instastory alichapisha video ikimuonesha yeye pamoja na Mimi Mars wakiwa studio wanarekodi huku Lunya akisikika akisema "Okay Alright lets get it, I got Mimi Mars on My album" na hivyo kuthibitisha kuwa Mars atakuwepo kwenye albamu hiyo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Aidha kwenye video hiyo, alikuwepo Quick Rocka pamoja na mtayarishaji muziki Ammy wave.

Kama wimbo huo utakamilika basi itakuwa ni kwa mara nyingine wasanii hao wameshirikana kufanya wimbo pamoja kwani mwaka 2018 Mimi Mars alimshirikisha Lunya kwenye wimbo wake wa ‘Sitamani’ ambao pia uliandikwa na Young Lunya.

Aidha kwa muda mrefu sasa, Young Lunya amekuwa akitoa mdokezo kuhusiana na albamu yake na wasanii watakaoshiriki kwenye albamu hiyo ambayo itakuwa ni albamu ya kwanza kutoka kwa Lunya tangu aanze safari yake ya muziki.

Soma Pia: Harmonize Kuachia Ngoma Nyingine Baada ya Mang'Dakiwe Kupata Mafanikio Makubwa

Tukianza na Aprili 25 mwaka huu, Lunya alichapisha picha akiwa na Diamond Platnumz pamoja na S2kizzy na kisha kuandika "BET y'all want Diamond in my album nipo nae hapa anything can happen" na taarifa hiyo ilichukuliwa na mashabiki kuwa kuna uwezekano Simba akashiriki kwenye album ya Mbuzi.

Ilipofika Juni 16 mwaka huu, Young Lunya kupitia ukurasa wake wa Instagram alithibitisha kuwa rapa kutoka kundi la Weusi Joh Makini atakuwepo na kudhiriki kwenye albamu yake.

Leave your comment