Nyimbo Mpya:Ngoma 5 Zilizoachiwa Bongo na Rayvanny, Marioo na Barakah the Prince

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bila shaka tutakuwa hatujakosea tukisema kuwa soko la muziki nchini Tanzania linazidi kunawiri siku baada ya siku kutokana na ukweli kuwa wasanii wanatoa kazi zenye viwango vya juu.

Soma Pia: Rayvanny Vs Mbosso:Nani Mkali Zaidi?

Wiki hii mambo hayajawa tofauti sana kwani wasanii kama Marioo, Barakah The Prince, Rayvanny, Mo Music na wengineo wametoa ngoma kali. Makala hii inaangazia nyimbo tano mpya zilizotoka wiki hii hapa nchini Tanzania:

Sweet - Rayvanny

Baada ya ‘Jeniffer Remix’ kufanya vizuri , Rayvanny anaungana kwa mara nyingine na msanii kutokea, nchini Nigeria Guchi kwenye ‘Sweet’. Wimbo wa ‘Sweet’ umeonesha ushirikiano ulioshiba kati ya Rayvanny na Guchi. Kwenye wimbo huu, wasanii hawa wanachukua nafasi ya wapenzi kwani wanatumia lugha ya kifasihi na maneno laini kila mmoja akimsifia mwenzake kwa mapenzi wanayopeana.

https://www.youtube.com/watch?v=ach6SBIUfs0

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Benpol Aachia EP Mpya ‘B’

Mo Music - Eva

Waswahili wanasema avumaye baharini papa na wengine pia wapo. Msanii Mo Music amezidi kuonesha kuwa bado yupo kwenye kiwanda cha muziki baada ya kuachia mkwaju wake mpya unaoitwa ‘Eva’. Kwenye ‘Eva’, Mo Music anamuelezea mpenzi wake kwa maneno mazuri akifafanua urembo na ulimbwende wa mpenzi wake na bila shaka wimbo huu ni makhususi kwa ajili ya wapendanao.

https://www.youtube.com/watch?v=1Nu10ayRE1U

Snake - Brian Simba & Chidi Benz

Nini kinatokea pale ambapo msanii mkongwe kama Chidi Benz anakutana kwenye wimbo mmoja na damu changa kama Brian Simba? Bila shaka ni wimbo mkali. Ndani ya ‘Snake’,  Brian Simba anatumia Hip-hop laini aina ya Trap kumsifia mwanamke ambaye ni fundi sana wa kucheza na miondoko ambayo inawapagawisha sana wawili hao.

https://www.youtube.com/watch?v=-12AxV1PWGg

Wow - Marioo

Marioo hajawahi kuwaangusha mashabiki zake na ndio maana kila mara akiachia wimbo lazima mashabiki waseme ‘Wow’. Kwenye ‘Wow’,  Marioo anaturudisha club kwenye kucheza dansi kwani Kimambo beats ambaye ndiye mtayarishaji wa kibao hiki ametumia mdundo uliochangamka huku Marioo akitumia sauti yake tamu kumshangaa na kumsifia mwanamke kutokana na alivyoumbika.

https://www.youtube.com/watch?v=Epy9fd9BisU

Rainey - Barakah The Prince & Skyfye

Nani kama Barakah The Prince kwenye suala ka kubembeleza na kulilia mapenzi? Kwenye kibao chake kipya kinachoitwa ‘Rainey’ Barakah anaendelea kujijengea heshima kwenye eneo hilo. Kwenye ‘Rainey’, Barakah anatumia sauti yake iliyotulia, kumbembeleza mwanamke ambaye tayari yuko kwenye mahusiano na mwanaume mwengine awe nae kimapenzi iwapo mwanamke huyo ataona mtu ambaye yuko kwenye mahusiano nae hamfai. Barakah yuko tayari kutumika kama ‘Spare Tyre’.

https://www.youtube.com/watch?v=Hg3iPfLXG-o

Leave your comment