Nyimbo Tano Kali Kutoka Tanzania Ambazo Zimekosa Video

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kwa miaka ya hivi karibuni video za muziki zimekuwa ni za muhimu kwa wasanii kwa kuwa video inawapawatazamaji fursa ya kutazama ujumbe wa msanii.

Soma Pia: Video 5 Zilizo na Watazamaji Wengi Zaidi YouTube Tanzania

Kila msanii kwa sasa hujitahidi ili kuachia video baaday ya kutoa wimbo mpya. Hata hivyo, kuna baadhi ya nyimbo ambazo zilifanya vizuri sana kwenye redio na mitandao lakini mpaka leo hazina video. Makala hii inaangazia Nyimbo tano kutoka Tanzania ambazo zimefanya vizuri lakini zimekosa video:

Soma Pia: Zuchu Aeleza Sababu ya Kuimba Muziki wa Singeli Kwenye ‘Nyumba Ndogo’

Far Away - Diamond Platnumz ft Vanessa Mdee

Kutoka kwenye albamu ya ‘A boy from Tandale’, wimbo wa ‘Far Away’ ni wimbo namba 18". Wimbo huu uliwakutanisha kwa mara ya kwanza Diamond na Vanessa Mdee ambaye kwa kipindi kile alitamba na albamu yake ya ‘Money Mondays’. Baada ya maswali kuwa mengi Vanessa Mdee aliweka wazi kuwa maswali kuhusu video ya wimbo huo aulizwe Diamond kwani yeye ndiye mwenye wimbo. Kufikia sasa, wimbo huo YouTUbe umetazamwa mara Laki Tano na thelathini na nne elfu.

https://www.youtube.com/watch?v=6JzBKTvIigg

Ashua - Zuchu ft Mbosso

‘Ashua’ ni wimbo namba 6 kwenye EP ya ‘Iam Zuchu’ na ndio wimbo pekee kwenye EP hio ambao umekosa video. Si Zuchu wala Mbosso ambaye alishawahi kueleza kwanini wimbo huu uliotayarishwa na Mocco Genius haujafanyiwa video. Kufikia sasa wimbo huu imepata kusikilizwa mara milioni mbil nukta nane kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=caYVX00bnXw

Lini - Navy Kenzo ft Alikiba

‘Lini’ ni wimbo ambao Navy Kenzo wamemshirikisha Alikiba na ni wimbo namba moja kwenye kwenye albamu ya Navy Kenzo inayokwenda kwa jina la ‘Above In A Minute’ iliyotoka mwaka 2017. Ni takriban miaka minne sasa imefika tangu wimbo huo utoke na hakuna hata dalili ya video ya wimbo huo.

https://www.youtube.com/watch?v=27rDsAUrJSU

Nivumilie - Ruby ft Barakah The Prince         

Wimbo huu ulitoka kipindi ambacho msanii Ruby yupo THT na Barakah The Prince alikuwa bado hajaingia Rockstar 4000. ‘Nivumilie’ ilitamba sana mwaka 2016 kutokana na mistari yake kugusa hisia za watu wengi lakini ulikosa video na Aprili mwaka jana Baraka aliweka wazi kuwa, video ya wimbo huo haikukamilika kwa sababu Ruby hakutoa ushirikiano wa kutosha.

https://www.youtube.com/watch?v=MtSiRNpWGts

Vumbi - Rayvanny ft Diamond Platnumz

Julai mosi mwaka 2019 Rayvanny alitoa wimbo wake unaoitwa ‘Vumbi’ akishirikiana na Diamond Platnumz. Pamoja na kukosa video, wimbo huu kufikia sasa umeshatazamwa takribani mara Milioni mbili nukta tatu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=_VoqFsJou3c

Leave your comment