Meneja wa WCB Sallam SK Aweka Wazi Bei ya Zuchu Kwenye Show

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Meneja wa muda mrefu wa Diamond Platnumz Sallam SK ameweka wazi kiasi ambacho msanii Zuchu analipwa kwa kufanya tamasha moja nje ya nchi. Kwenye mahojiano aliyoyafanya kwenye kipindi cha The Switch kinachoruka Wasafi Fm, Sallam aliweka wazi kuwa ili promota aweze kumpata Zuchu kwa tamasha la nje ya nchi inabidi alipe kiasi cha dola 20,000 za kimarekani.

Soma Pia: Zuchu Azungumzia Mafanikio Yake Mwaka Mmoja Kwenye WCB

"Zuchu bei yake imebadilika sana tu, iko dollar 20,000 ( Milioni 46 za kitanzania)" alitanabaisha meneja huyo.

Hata hivyo Sallam alitoa tahadhari kuwa kiasi hicho ni kwa zile shows za nje ya nchi lakini kwa shows za ndani, kiwango kitabadilika na kuwa pungufu ya hapo kwa sababu Tanzania ni nyumbani hivyo hawana haja ya kuweka tozo kubwa.

"Local shows tunaangalia, tunaongea lakini haiwezi kupungua sana za nyumbani ni nyumbani kwa sababu huwezi kuwanyima watu wa nyumbani," alidokeza Sallam.

Soma Pia: Zuchu Atangaza Ujio wa Tamasha la ‘Zuchu Homecoming’ Mwezi Ujao Zanzibar

Ikumbukwe kuwa pamoja na bei ya msanii Zuchu kuonekana kuwa kubwa, msanii huyo ndani ya muda mfupi tu ameweza kujitengenezea jina kwa kutoa nyimbo zilizopendwa na mashabiki kama "Sukari" , "Cheche". "Litawachoma" na "Nyumba Ndogo" huku EP ya "I am Zuchu" iliyotoka April mwaka jana ikitengeneza rekodi mbalimbali kwenye mitandao ya kusikiliza na kuuza muziki.

Sallam pia alitumia fursa hiyo kugusia tamasha la msanii Zuchu "Zuchu Homecoming" linalotegemewa kufanyika Agosti 21 mwaka huu uwanja wa Amani pale Visiwani Zanzibar kwa kuwahasa wafanyabiashara na kampuni tofauti kudhamini tamasha hilo kwani kampuni ikitangaza kupitia tamasha itasaidia kukuza soko la kampuni husika.

Leave your comment