Snoop Dogg Amshauri Diamond Jinsi ya Kuwa Bora Kimuziki

 [Picha: Diamond Platnumz | Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Hivi karibuni mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz alikutana na rapa wa Marekani Snoop Dogg. Wawili hao walizungumza kuhusu masuala mbali mbali kwenye tasnia ya muziki.

Diamond alichapisha picha ambazo zilimuonyesha akiwa pamoja na Snoop Dogg. Bosi huyo wa WCB alisema kuwa ni vizuri kupata ushauri kutoka kwa wale ambao wamefanikiwa zaidi na wako na uzoefu pia.

Soma Pia: Wasanii 5 Wenye Wafuasi Wengi Zaidi Kwenye YouTube Tanzania

Video fupi iliyoibuka kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha Snoop Dogg akimpa ushauri Diamond jinsi ya kupanda ngazi kwenye tasnia ya muziki na kufanikiwa zaidi kama msanii.

Snoop Dogg alimwambia Diamond aache kuzingatia idadi ya wafuasi au watazamaji ambao nyimbo zake hupata. Alimuelezea kwamba wakati mtu atazingatia nambari, atahisi kama hafanyi maendeleo na atakata tamaa katika mchakato huo.

Rapa huyo pia alimwambia Diamond kuwa asitishwe wakati wasanii wengine wataanza kuimba kama yeye au kumuiga, ila anapaswa kujivunia. Kulingana na Snoop Dogg, ilikuwa ni motisha sana kuona msanii kutoka Tanzania, Afrika akiinuka na kufikia kiwango alichokuwa Diamond.

Soma Pia: Zuchu Aeleza Sababu ya Kuimba Muziki wa Singeli Kwenye ‘Nyumba Ndogo’

Alimsifia Diamond na kumsihi afanye bidii zaidi. Diamond wakati wa mkutano huo alikuwa msikivu na mnyenyekevu sababu alikuwa amepta fursa ya kipekee ya kukutana na kuzungumza na mmoja wa wanamuziki wanaoheshimika zaidi ulimwenguni.

Diamond bado yuko Marekani ambapo anafanya kazi kwenye albamu yake inayotarajiwa kuachiwa hivi karibuni.

Leave your comment