Zuchu Aweka Rekodi Mpya, Afikisha Jumla ya Watazamaji Milioni Mia Mbili Kwenye YouTube

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa WCB Zuchu ametoa shukrani kwa mashabiki wake kwa kumuunga mkono na kumwezesha kufikia watazamaji milioni 200 kwenye mtandao wa YouTube. Hii ni rekodi mpya Afrika Mashariki kwa wasanii wa kike.

Zuchu amekuwa akifanya kazi katika tasnia ya muziki wa Tanzania kwa takriban mwaka mmoja na amefanikiwa sana kama msanii ndani ya kipindi hicho.

Soma Pia: Zuchu ‘Sukari’ na Video Zingine za Wasanii wa Kike Bongo Zilizotazamwa Zaidi YouTube

Mwimbaji huyo pia ana zaidi ya wafuasi milioni moja kwenye YouTube na wafuasi takriban milioni tatu kwenye mtandao wa Instagram. Idadi hiyo kubwa ya wafuasi ni uthibitisho tosha kwamba Zuchu ni miongoni mwa wanamuziki wenye ushawishi mkubwa nchini Tanzania.

Zuchu kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii alisema kuwa anawapenda mashabiki wake na anashukuru kwa uungaji mkono na upendo ambao walikuwa wamemuonyesha kimuziki.

 "200,000,000 million total viewers on @Youtubemusic thank you for your endless support .Wow I just love you all so much," Zuchu aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano za Zuchu, Diamond, Alikiba na Rayvanny Zinazovuma YouTube

Zuchu alipata umaarufu zaidi na kujipatia heshima kubwa katika tasnia ya muziki na wimbo wake wa Sukari ambao ulivuma sana kwenye mtandao. Sukari ni miongoni mwa nyimbo zinazotazamwa na kusikilizwa zaidi kutoka kwa Zuchu. Wimbo huo hadi sasa una watazamaji zaidi ya milioni arobaini na tano kwenye YouTube.

Wimbo wa Zuchu wa hivi karibuni ulioitwa ‘Nyumba Ndogo’ pia umepokelewa kwa upendo mwingi kati ya mashabiki. Nyumba Ndogo inafanya vizuri na imepata watazamaji takriban milioni nne ndani ya wiki moja.

Leave your comment