Nyimbo Mpya: Ngoma Tano za Zuchu, Diamond, Alikiba na Rayvanny Zinazovuma YouTube

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki ya pili ya mwezi Julai imeshawadia na imekuwa ni wiki ambayo kumekuwa na purukushani nyingi sana kwenye kiwanda cha muziki hapa nchini Tanzania kwani nyimbo kali sana zimeachiwa kutoka kwa wasanii tunaowapenda.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Pasi na shaka utakuwa umeshasikiliza na kuona video nyingi za wasanii zimetoka wiki hii ila zifuatazo ni nyimbo tano zinazoendelea kufanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa YouTube:

Soma Pia: Zuchari ‘Sukari’ na Video Zingine za Wasanii wa Kike Bongo Zilizotazmwa Zaidi YouTube

Nyumba ndogo – Zuchu

Kwa wiki ya pili mfululizo video ya ‘Nyumba Ndogo’ kutoka kwa malkia wa WCB Zuchu inaendelea kushika namba moja kwenye nyimbo zilizofanya vizuri zaidi YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=KsU31FyvFxY

Ex Wangu remix - Hamisa Mobetto ft Seneta Kilata

Licha ya kuwa mara yake ya kwanza kuimba muziki wa Singeli, Hamisa Mobetto hajawaangusha mashabiki zake. Kufikia sasa, video ya wimbo huu imetazamwa takriban mara milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=CmSgffQYaSo

Jeniffer Remix - Guchi ft Rayvanny

Kutokea nchini Nigeria, msanii Guchi anaungana na mkurugenzi mtendaji wa Next Level Music Rayvanny kwenye Jeniffer Remix. Video ya wimbo huu imefanyika Tanzania na imeongozwa na Eris mzava. Ndani ya siku nne tu, video imeshatazmwa mara Milioni moja nukta saba kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=2bXXaiwh1Zg

Salute - Alikiba ft Rude Boy

Wapenda muziki mzuri wameendelea kumpigia ‘Salute’ msanii Alikiba ambaye kwenye wimbo huu ameshirikiana na Rude Boy kutokea nchini Nigeria. Ni ukweli usiopingika video ya wimbo huu ina stori nzuri na ya kuvutia sana na kufikia sasa video ya wimbo huu imeshatazamwa mara milioni tatu nukta nane huko YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=oQ8SycSejrM

Kamata - Diamond Platnumz

Mpaka sasa, video ya wimbo huu imetazamwa mara milioni nne nukta moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=0dtdfKEoMuU

Leave your comment