Zuchu ‘Sukari’ na Video Zingine za Wasanii wa Kike Bongo Zilizotazamwa Zaidi YouTube

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Siku mbili zilizopita msanii Zuchu kutokea WCB aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kike aliyetazamwa sana kwenye mtandao wa Youtube Afrika Mashariki baada ya video zake zote kutazamwa takriban mara Milioni 200 kwenye mtandao huo.

Soma Pia: Diamond Platnumz Akutana na Snoop Dogg Katika Ziara yake Marekani

Makala hii imelenga kuonesha video za muziki za wasanii wa kike kutokea Tanzania zilizotazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Aslay Aachia Ngoma Mpya ‘Shangingi Mtoto’

Sukari – Zuchu

Video ya wimbo wa Sukari ilitoka Januari 30 mwaka 2021 na iliongozwa na Kenny kutokea Zoom Extra. Kufikia sasa video hii imeshatazamwa mara Milioni 44 kwenye mtandao huo ikiwa ni miezi sita tangu kuachiwa kwake.

https://www.youtube.com/watch?v=CCmItvVgn6Q

Cheche - Zuchu ft Diamond Platnumz

Video ya Cheche ni mojawapo kati ya video zilizopendwa sana na mashabiki kutokana na miondoko yake ya kucheza.. Kufikia sasa video ya ‘Cheche’ imetazamwa mara Milioni 22.

https://www.youtube.com/watch?v=vyUslddxOpI

Iokote - Maua Sama

Akishirikiana na msanii mchanga Hanstone, Maua sama alitoa video ya Iokote October 6 mwaka 2018. Kazi ya kuongoza video hii alipewa Director Hanscana kutokea Hanscana Brand. Kufikia sasa video hii ishatazamwa mara Milioni 22.

https://www.youtube.com/watch?v=cyjeo2QUL_I

Litawachoma - Zuchu ft Diamond Platnumz

Kwenye wimbo huu, Zuchu anashirikiana kwa mara nyingine na Diamond Platnumz ambaye ndiye mkuu wa WCB. Kufikia sasa video ya wimbo huu imetazamwa mara Milioni 17 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=g9spgkHS2bs

Kivuruge - Nandy

The ‘African Princess’ anaingia kwenye orodha hii na wimbo wake wa ‘Kivuruge’ uliotoka Disemba 19, 2017. Video ya wimbo huu iliongozwa na Director Msafiri kutokea Kwetu Studios na kufikia sasa ishatazamwa takriban mara Milioni 13 huko YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=DAkFBWnwEcc

Leave your comment