Harmonize Aachia Kionjo cha Wimbo Wake Mpya wa Amapiano [Video]

[Picha: Harmonize | Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu Tanzania Harmonize ametangaza kuwa hivi karibuni ataachia wimbo mpya. Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alichapisha video ambao ulimwonyesha akifurahiya na kuimba wimbo huo mpya.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Wimbo Wake ‘Sandakalawe’

Kazi hiyo mpya imechukua mtindo wa mdundo wa Afrika Kusini ya Amapiano. Wimbo huo utakaoachiwa na Harmonize hautakuwa wa asili bali ni remix. Wimbo asili unakwenda kwa jina la Mang'Dakiwe na ulitayarishwa na DJ Obza kwa kushirikiana na Leon Lee.

Mdundo wa wimbo asili pia iko katika mtindo wa Amapiano. Mang'Dakiwe hadi sasa umepata watazamaji zaidi ya milioni nne kwenye mtandao wa YouTube. Idadi hiyo ni thibitisho tosha kuwa Mang'Dakiwe ulipokelewa vizuri na mashabiki.

Kulingana na Harmonize, anahitaji maoni 10,000 katika chapisho lake kwenye mtandao wa Instagram ili atoe remix ya Mang'Dakiwe pamoja na Dj Obza na Leon Lee.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aaachia Ngoma Mbili Mpya ‘Kazi Iendelee’ na ‘Tuvushe’

"The club one more time dem deady 10000 comments I’m dropping this remix @djobza_za ft free wifi kondeboy stay conected," chapisho la Harmonize lilisoma.

Tangazo la Harmonize linakuja muda mfupi baada ya wimbo wake ‘Sandakalawe’ kufanikiwa na kupokea watazamaji wengi kwenye mtandao wa YouTube.

Wimbo wa ‘Sandakalawe’ hivi sasa una watazamaji zaidi ya milioni tano ndani ya wiki moja ya uchapisho wake. ‘Sandakalawe’ pia ilikumbwa na utata huku mashtaka yakiibuka dhidi ya Harmonize kwamba alikuwa amenunua watazamaji wa wimbo huo.

Taza Video HAPA.

 

Leave your comment